kwenye taarifa iliotolewa na Ikulu ya rais jijini Dar es Salaam ikinukuu taarifa rasmi iliotolewa na kaimu balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Balozi Francis Mwaipaja, imekanusha vikali habari iliochapishwa na gazeti la serikali la news of Rwanda likidai kuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa na mazungumzo ya siri na viongozi wa kundi la FDLR la Rwanda.
Gazeti hilo hivi karibuni liliandika habari zinazodaikuwa kwa nayakati tofauti rais Kikwete amekuwa na mazungumzo jijini Dar Es Salaam na waanzilishi wa chama cha National Congress NRC, Dr Theogene Rudasingwa kamanda wa kundi la Democratic Forces of Liberation of Rwanda FDLR, luteni Kanali Wilson Irategeka, Kanali Hamadi pamoja na aliyekuwa waziri mkuu wa Rwanda Faustin Twagiramungu.
Kufuatia habari hiyo, Serikali ya Tanzania imemuandikia barua mhariri wa gazeti la News of Rwanda kumtaka aombe radhi pamoja na kuacha kuandika habari za uvumi ambazo kwa sehemu kubwa zimemuhusu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr, Jakaya Mrisho Kikwete.
Taarifa hiyo ambayo nakala yake rfikiswahili inayo, imekanusha kuwa mkutano kati ya rais Kikwete na viongozi hao ulifanyika tarehe 23 ya mwezi huu na kwamba tarehe hiyo rais Kikwete alikuwa safarini mjini Davos, Uswis kuhudhuria mkutano wa kiuchumi.
Wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania pia imekanusha kutoa pasi za kusafiria wala kuishi nchini humo kwa viongozi waliotajwa kuwa na mazungumzo na rais Kikwete.
Tangazo la Serikali ya Tanzania kukanusha taarifa hizi linakuja huku kukiwa imepita miezi kadhaa toka kuwepo kwa taarifa kuwa nchi hizo mbili zimekuwa kwenye mvutano kwa madai kuwa Tanzania inawasaidia waasi wanaompinga rais Paul Kagame.
0 comments: