Nyota wa muziki wa mtindo wa kufokafoka Kanye West na mwanamitindo Kim Kardashian wanatarajia kufunga ndoa miezi michache ijayo.
Hilo limethibitishwa na Kim Kardashian katika kipindi cha runinga kinachoendeshwa na Ellen DeGeneres.
Katika mahojiano hayo Kim aweka wazi kuwa atafunga ndoa na Kanye, na ndoa hiyo itafanyika nje ya Marekani; japo hakutoa tarehe rasmi ila alisisitiza si muda mrefu itafanyika.
Ellen alizidi kumchokonoa ili afunguke,ila Kim alizidi kusema bado hawajapanga tarehe rasmi.
Kanye West alifanya "suprise" kwa Kim katika sherehe za siku ya kuzliwa ya Kim kwa kumjulisha kwamba wangefunga ndoa.
Hellen alimpatia Kim zawadi ya ndoa kabla, alimzawadia nguo za ndani za kuogelea.
0 comments: