Kiungo wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ujerumani, Mesut Ozil. |
Kiungo mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaaka Ujerumani kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Ozil aliyesajiliwa na Arsenal akitokea Real Madrid kwa dau la paundi milioni 42 amewashinda Wajerumani wenzake wawili wanaotokea klabu ya Bayern Munich Philipp Lahm na Thomas Muller.
Ozil alipata asilimia 30% ya kura akifuatiwa na Philipp Lahm mwenye asilimia 17% na Thomas Muller asilimia 13%.
Ozil anaiona tuzo hiyo kama chachu ya ushindi wa Ujerumani kombe la dunia 2014 Brazil. Aliliambia shirikisho la soka Ujerumani "2013 ulikua muda mzuri wa kwangu kuhama kutoka Madrid kwenda London".
"Tuzo hii inanifanya niwe na furaha sana kwani ni tuzo ya mashabiki wa soka, na inanilazimu kufanya vizuri katika kombe la dunia 2014''
0 comments: