Robi Van Persie: |
Imeripotiwa kuwa Robin van Persie ataendelea kuwa nje kwa wiki sita zaidi. Majeraha aliyoyapata ya paja ni kama yale yaliyomweka nje muda mrefu akiwa Arsenal na Manchester United hawataki kumrudisha uwanjani mapema ili wasije wakampoteza kabisa.
Kwa sasa anaendelea na mazoezi na kocha wa viungo wa Timu ya PSV Eindhoven nyumabani kwao Uholanzi.
Kwa mujibu wa Gazeti la Dail Mail, Van Persie ambaye hajavaa uzi wa Manchester United tangu desemba 10,anaweza asionekane tena mpaka katikati ya mwezi wapili; japo David Moyes hataki kusema siku rasmi atakayorudi uwanjani.
Moyes alisema: "Tunajaribu kumrudisha lakini inatubidi tuwe makini isije ikajirudia hali kama iliyomkuta akiwa Arsenal.
"Yuko Uholanzi akishughulikiwa na mtu wanaejuana vizuri na sisi tunafanya kila tuwezalo ili kumrusha uwanjani"
0 comments: