Robin Van Persie na Wayne Rooney: |
Washambuliaji Wayne Rooney na Robin van Persie wote wa Manchester United, kuukosa mchezo dhidi ya Chelsea jumapili hii.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily mirror , Bosi wa Manchester United David Moyes; amethibitisha kutokuwepo kwa nyota hao kwenye mtanange huo japo wanaendelea vizuri.
Wayne Rooney ameonekana leo akifanya mazoezi na wenzake japo bado hajawa sawa kimchezo.
Inatarajiwa huenda Robin Van Persie akarudi mazoezini wiki ijayo na kurudi uwanjani mwisho wa mwezi huu.
David Moyes alisema kwamba: "Wayne hayuko tarari kwa mchezo dhidi ya Chelsea,"
"Amekuwa akiendelea na mazoezi ya kukimbia, na leo nimemuona akikimbia, kwakweli hali yake inaridhisha".
0 comments: