Luis Suarez |
Luis Suarez amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa 12 ligi kuu ya Uingereza baada ya kuonyesha kiwango safi.
Mshambuliaji huyo nguli wa Liverpool alitikisa nyavu mara 10 katika mwezi wa 12 wakiwa wamecheza na Norwich, West Ham, Tottenham na Cardiff.
Kwa upande mwingine Bosi wa Manchester City Manuel Pellegrini amezawadiwa tuzo ya kocha bora wa mwezi. Manchester City chini ya Pellegrini ilichukua pointi 16 kati ya kumi na 18 ambazo wangeweza kuchukua mwezi wa 12.
Manuel Pellegrini |
0 comments: