Kocha wa Chelsea Jose Morihno: |
Kocha mreno mwenye machachari mengi Jose Mourinho amekarirwa na Gazeti la Daily star akisema kwamba hana mpango wa kuondoka Stamford Bridge. Mourinho amesema yupo Chersea kwa muda mrefu na inawezekana akatundika daruga akiwa katika klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la London.
"Sifikirii nitakwenda wapi baada ya hapa sababu sina mpango wa kuhama" alisema Mourihno. Alirudi Stamford Bridge msimu huu baada ya kuwa nje kwa miaka sita na amekua na matokeo mazuri tangu arejee.
"Nitaondoka hapa pale tu ambapo Chelsea itaamua kua muda umefika mimi kuondoka".
"Nilipofanya maamuzi ya kurudi Chersea sikufahamu kama wangenikaribisha lakini walifanya hivyo". "Nyumba yetu iliyoko London tuliitunzi tukijua siku moja tungerudi London japo sikusema"
0 comments: