Mkongwe Giggs wa manchester United akipachika bao golini kwake |
Sunderland waliokuwa nyumbani imeendeleza ubabe unaoanza kuonyeshwa na timu mbalimbal kwa mashetani wekundu.
Katika uwanja wao wa nyumbani, Sunderland walikuwa wa kwanza kupachika bao; Jonny Evans alisababisha faulo iliyopigwa na Sebastian Larsson. Katika purukushani za kuokoa mchomo huo mkongwe Rayan Giggs akatumbukiza mpira nyavuni kwao.
Dakika sita baada ya kipindi cha pili kuanza, Mlinzi wa kati Nemanja Vidic aliweza kusawazisha kwa mpira mzuri wa kichwa.
Mwamuzi Andre Marriner alitoa penalt iliyosababishwa na Cleverley. Borini hakufanya kosa baada ya kupewa fursa ya kuihukumu United na kumaliza mchezo 2 - 1.
Borin akipiga mkwaju wa penaiti uliowauwa United |
0 comments: