Kiungo wa Arsenal Searg Nabri |
Boss wa Wigan Uwe Rosler, anamuhitaji kiungo Mjerumani wa Arsenal Gnabry. Hilo limekuja baada ya kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low kudai kwamba kijana huyo mwenye umri wa mika 18 anafuatiliwa vilivyo ili ikiwezekana ajumuishwe kwenye kikosi cha kombe la dunia 2014. Hivyo anahitaji kucheza michezo mingi. Hivyo Boss wa Wigan Uwe Rosler anadhani anaweza kuipata saini ya kinda huyo kwa mkopo dilisha dogo la usajili januari.
Mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke |
Kwa mujibu wa Gazeti la maka, klabu ya soka Atletico wenye makazi yao katika mji wa Madrid Hispania; wanaiwindi saini ya mfumani nyavu wa Aston Villa Christian Benteke.
Beki wa kushoto wa Chelsea Ashley Cole |
Beki wa Chelsea Ashley Cole, Anawindwa na magwiji wa mji wa Madrid; Real Madrid. Na hili litafikiwa endapo tu Fabio Coentrao ataondoka katika klabu hiyo.Habari kwa hisani ya(The Express).
Mshambuliaji wa Sunderland Stevene Fletcher |
Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, Meneja wa Hull City Steve Bruce atenga poundi milion 6 kwa ajili kumwania mshambuliaji wa Sunderland Steven Fletcher.
Fletcher aliifungia Sunderland bao la kusawazisha akitokea benchi katika mech dhidi ya Cardiff City iliyoishia sare ya bao 2 - 2.
Verona Jorginho |
Liverpool wananyatia saini ya kiungo wa kati wa Verona, Jorginho; ameifungia timu yake mabao 7 na kutengeneza nafasi 23. Habari kwa hisani ya ( talkSPORT).
Nemanja Matic |
Manchester City wako tayari kumtoa Javi Garcia pamoja na paoundi milioni 20 kwa Benfica kuinasa naisi ya Nemanja Matic. Habari kwa mujibu wa The Mirror.
Koke |
Manchester United wako tayari kutoa kitata cha pound milioni 25 kuinasa saini ya kiungo wa Atletico Madrid Koke, kwa mujibu wa The Metro.
John Heitinga |
Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror Norwich City wanafukuzia saini ya John Heitinga.
Mshambuliaji wa Hannover 96 Mame Diouf |
Stoke City inajaribu kuandaa fedha ili kumnasa mshambuliaji wa kati wa Hannover 96 Mame Biram Diouf, kwa mujibu wa The Sentinel.
Mathieu Valbuena |
Kiungo wa Marseille Mathieu Valbuena anafuatiliwa na meneja wa timu ya Arsenal Arsen Wenger, pamoja na Napoli na Atletico Madrid.Kwa mujibu wa gazeti la Hispania El Mundo Deportivo.
Hata vivyo yoso wa Brazilian Wellington Silva aliyejiunga na Arsenal tangu mwaka 2010, na kukosa kibali cha kufanyia kazi Uingereza tayari anaweza kuingia Arsena baada ya kutimiza umri wa miaka 20.
0 comments: