Oliver Gilroud akishangilia goli lake la pekee katka mchezo wa ligi kuu uingereza baina ya Newcastle na Arsenal |
Bao la pekee la Olivier Giroud dhidi ya Newcastle limetosha kuirudisha Arsenal kileleni mwa ligi kuu ya uingereza.
Arsenal walicheza bila ya kuwepo Mesut Ozil, ila Jack Wilshere na Laurent Koscielny walirejea kikosini. Alan Pardew, alimuanzisha Cheick Tiote na kumwacha Hatem Ben Arfa nje.
Newcastle walikaribia kupachika bao baada ya Moussa Sissoko kuachia shuti kari lililookolewa na mlinda mlango Wojciech Szczesny, na kwa wakati mwingine kichwa kizuri cha Mathieu Debuchy kugonga mwamba.
Hata hivyo Arsenal ilipata goli dakika ya 65 kupitia mshambuliaji wake Olivier Giroud alieunganisha vizuri faulo iliyopigwa na Theo Walcot. Arsenal inaongoza ligi ikiwa na pointi 42 mbele ya Man City yenye pointi 41.
Jack Wilshere wa Arsena na Sheikh Tiote wa newcastle wakigombea mpiri kwenye mech baina ya Newcastle na Arsenal |
0 comments: