kiungo wa Hull City Tom Huddleston akinyolewa nywele na daktari wa timu Rob Price baada ya kuifungia timu yake goli |
Kiungo wa Hull City Tom Huddlestone hatimaye alivunja ukame wake wa kupachika mabao, na kuamua kukata nyele zake.
Mchezaji huyo wa zamani wa Spurs alikuwa hajaziona nyavu kwa zaidi ya mwaka mpaka jana katika mchezo dhidi ya Fulham, kutokana na ukame huo aliahidi kutonyoa nywele zake mpaka pale atakapofunga bao.
Baada ya kufunga goli jana katika uwanja wa KC alikimbia moja kwa moja kwenye benchi la ufundi na kumwomba daktari wa timu Rob Price amnyoe nyele kidogo kutumia mkasi wa kufanyia upasuajia.
Hata hivyo goli hilo lilikuwa kama zawadi yake ya siku ya kuzaliwa kwani jana alifikisha miaka 26.
Hull iliipiga Fulham magoli 6 - 0.
Wachezaji wa timu ya Hull City wakishangilia goli lililopachikwa na Tom Huddlestone |
0 comments: