Dec 26, 2013

MAN UNITED ,ARSENAL NA CHELSEA ZAENDELEZA UBABE

Posted at  12/26/2013  |  in  Michezo

wachezaji wa manchester united wakishangilia ushindi
Klabu ya Manchester United imetoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 dhidi ya Hull City Uwanja wa KC, huku mchezaji wa zamani wa Mashetani hao Wekundu James Chester akijifunga kuamua mshindi.Chester alitangulia kuifungia Hull dakika ya nne, Meyler akafunga la pili dakika ya tatu na Man United ikazinduka na kupata bao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Smalling, pasi ya Rooney aliyefunga la kusawazisha dakika ya 26.Man United ilijihakikishia pointi tatu dakika ya 66 baada ya Chester kujifunga. 


Katika mchezo mwingine, bao pekee la Edin Hazard dakika ya 29 liliiipa ushindi wa 1-0 Chelsea dhidi ya Swansea Uwanja wa Stamford Bridge.



Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Boleyn, mabao ya Theo Walcott dakika ya 68 na 71 na Lukas Podolski dakika ya 69. Bao pekee la West Ham limefungwa na Cole dakika ya 46.

shambuliaji wa arsenal lucas podolski akishangilia ushindi

Aston Villa imefungwa 1-0 na Crystal Palace, Cardiff City imefungwa 3-0 na Southampton, Everton imefungwa 1-0 nna Sunderland, Newcastle United imeifumua 5 - 1 Stoke City, Norwich City imefungwa 2-1 na Fulham na Tottenham Hotspur imetoka sare ya 1 - 1 na West Bromwich.

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 mchambuzi@habari online. Blogger Template by Bloggertheme9
Proudly Powered by Blogger.
back to top