Dec 30, 2013

yanga kusajili kocha mwingereza

Posted at  12/30/2013  |  in  Michezo

Nembo ya dar es salaam young Africans

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga, mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji na mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya kimataifa, Seif Ahmed ‘Magari’ walikwea pipa kuelekea mjini London kwa ajili ya kusaka kocha mpya wa timu hiyo Yanga.

Kwa taarifa zilizomo ndani ya wanajangwani hao,kesho uongozi utakutana kabla ya kukutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuweka wazi mambo mbalimbali likiwemo suala la kocha mkuu.
Masuala mengine ambayo yatajadiliwa ni hatima ya kocha msaidizi, Fred Minziro ambaye inasadikiwa nafasi yake itachukuliwa na kocha mkuu, Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa.
Pia mkutano huyo utatoa hatma ya ushiriki wa Yanga katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi na safari ya Hispania kwa ajili ya kambi.
Mpaka sasa hakuna anayejua kama Yanga itashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuwa timu hiyo ina mpango wa kuweka kambi nchini Hispania au Uturuki.
Iwapo Yanga watashiriki Kombe la Mapinduzi litalomalizika Januari 13, watakuwa na siku 10 za kujiandaa nje ya nchi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara  iliyopangwa kuanza Januari 25.
Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji
Mwenyekiti wa yanga Yusuf Manji

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 mchambuzi@habari online. Blogger Template by Bloggertheme9
Proudly Powered by Blogger.
back to top