Jan 15, 2014

Kesi yaanza kusikilizwa mauaji ya West Gate Kenya

Posted at  1/15/2014  |  in  Habari


shambulio la west gate kenya
Wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuwahifadhi waliofanya tukio la ushambuliaji Westgate Kenya:

Kesi ya shambulio la West Gate yaanza kusikilizwa Jijini Nairobi nchini Kenya, ikihusisha vijana wanne wanaotuhumiwa kwa kosa la kutoa hifadhi kwa washambuliaji.
Watuhumiwa hao wamepinga mashtaka yaliyo juu yao, shitaka la kuwahifadhi magaidi na kuingia nchini Kenya kinyamela.
Mahakama ilisikiliza maelezo ya mlinzi aliyekuwa akilinda nje ya Westgate pindi ilipovamiwa.
Kwa mujibu wa BBC Africa, Mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina la Stephene Juma; aliiambia mahakama kwamba alikuwa akiongoza magari nje ya westgate kabla ya gari moja kusimama na watu watatu kuruka kutoka ndani ya gari hilo. Aliongezea kwamba hakuona sura zao ila alianza kusikia milio ya risaisi ghafla.
"Niliata msaada kupitia redio niliyokuwa nayo na kujihifadhi jirani nikisubiria polisi wafike eneo la tukio"
Ripoti toka ppolisi zinadai kwamba washambuliaji hao walihifadhiwa na watuhumiwa hao katika makazi yao yaliyo Eastleigh Nairobi. Mbali na kuwahifadhi, kumekuwa na mawasiliano baina yao siku nne kabla ya shambulio hilo.
Mmoja wa watuhumiwa wa shambulio hilo ni kijana Msomalia aliyezaliwa Norway mwenye umri wa miaka 23 anayefahamika kwa jina la Hassan Abdi Dhuhulow.
Kikundi cha al-Shabab  cha Somalia chenye uhusiano wa karibu na al-Qaeda  kimesema kwamba tukio hilo lilifanywa na wapiganaji wake. 
Kikundi cha al-shabab kinaitaka serikari ya Kenya iondoe majeshi yake nchini Somalia.

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 mchambuzi@habari online. Blogger Template by Bloggertheme9
Proudly Powered by Blogger.
back to top