Tajiri kuliko wote nchini China Wang Jianlin, ajiandaa kuweka mezani kitita ili kuinyakua Southampton.
Ikiwa atafanikiwa basi itamaanisha Nicola Cortese atarudi Southampton kama mwenyekiti wa klabu hiyo.
Inasemekana meneja wa klabu hiyo Mauricio Pachettino, anaijua nia ya Billionea huyo kiongozi wa kampuni ya uwekezaji ijulikanayo kwa jina la Wanda.
Kampuni ya Wanda ina utajiri wa Billiona 175, nusu ya utajiri huo ukiwa ya Wang Jianlin.
Jianlin anadhamiria kuingia katika ligi kuu ya Uingereza ili kuitangaza zaidi kampuni yao ya Wanda, kwa kumwanga mezani paundi millioni 175; ambayo itamfanya mmiliki wa sasa Liebherr asiwe na ujanja mwingine zaidi ya kulikubali donge hilo.
Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la Daily Mirror, mazungumzo ya dili hilo yameshaanza na yanaelekea kufanikiwa.
Iwapo dili hilo litakamilika litaifanya Southampton kuwa klabu tajiri zaidi katika ligi kuu ya Uingereza.
0 comments: