Jan 4, 2014

Miyeyusho amtwanga Mkenya

Posted at  1/04/2014  |  in  Michezo

mchezo wa ngumi
Bondia Francis Miyeyusho (kulia) akimtupia konde mpinzani wake, Joshua Amakulu . Picha na MWANANCHI

Bondia, Francis  ‘Chichi mawe’ Miyeyusho juzi usiku  aliibuka kinara baada ya kumgaragaza  Joshua Amukulu wa Kenya kwa Knock  Out (KO) raundi ya pili ya pambano  la raundi nane la uzani wa light. Katika pambano hilo lililopigwa  kwenye Ukumbi wa Msasani Club jijini  Dar es Salaam, Miyeyusho alionekana  yuko imara tangu kengele ya  kuashiria kuanza kwa raundi ya  kwanza ya pambano hilo.
Amukulu ndiye alikuwa wa kwanza  kurusha konde katika raundi hiyo na  Miyeyusho kukwepa na kujibu  mashambulizi yaliyodumu hadi dakika  tatu za raundi ya kwanza  zinamalizika.
Hali ilikuwa tete kwa Amukulu raundi  ya pili ya pambano hilo ambapo kabla  ya kengele ya kuashiria kumalizika  kwa dakika tatu za raundi hiyo,  konde la Miyeyusho lilimpotezea  mwelekeo mpinzani wake ambaye  alishindwa kuendelea na pambano na  mwamuzi kutoa ushindi wa KO kwa  Miyeyusho.
“Ni matokeo ambayo niliyatarajia  kutokana na maandalizi niliyofanya,  nilisema tangu mwanzo kuwa ‘hapa  lazima ukae’ ndivyo ilivyokuwa kwa  huyu Mkenya, hili ni fundisho kwa  mabondia wengine pia,” alitamba  Miyeyusho.

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 mchambuzi@habari online. Blogger Template by Bloggertheme9
Proudly Powered by Blogger.
back to top