Jan 17, 2014

Chadema yaweka wazi majina ya wagombea wa udiwani kanda ya kaskazini

Posted at  1/17/2014  |  in  Habari

wagombea wa chadema

Tarehe 15 Januari 2014, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za kanda ya Kaskazini.
Wagombea hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.
Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:
JINA LA MGOMBEA
KATA
JIMBO
MKOA
BI. MWANAISHA MOHAMED OMARI
KIOMONI
TANGA DC
TANGA
BW. KAGOMA FRANK HENRY
KIBORLONI
MOSHI MJINI
KILIMANJARO
BW. ALLY BANANGA
SOMBETINI
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. CHARLES SAMWEL MGATA
PARTIMBO
KITETO
MANYARA
BW. SANING’O KONE
LOLERA
KITETO
MANYARA
Katika uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana tukiwa na uhakika kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao kwa kuzingatia uwezo wa wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana na kuwatumikia wananchi na dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za wananchi zilizoletwa na CCM kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.
Aidha chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa kumteka mgombea wa CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya tarehe 15.01.2014 muda mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa. Tukio hili limetokea huku tukiwa na taarifa zilizopatikana baadae kuwa mida ya saa nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa na kiongozi mmoja wa CCM wa wilaya.
Uongozi wa kanda tumesharipoti tukio hili polisi na kupewa RB namba LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea kwa ndg ALLY SAIDI JAHA. Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo umeshwandikia barua msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na kupotea kwa mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili kwa kina chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.
Hivi sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa kushirikiana na Red Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili ambalo limetufedhehesha sana na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya kiongozi na chama wanachokitaka. 
Niwahakikishie wakazi wa Mtae na Watanzania wote wapenda mabadiliko ambao jambo hili limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi Jaha atatafutwa mpaka apatikane akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini kimemtokea na pia awaeleze watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini nyuma yake. Hapa kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili jambo halitaisha kirahisi hivi hivi.
Niwaombe wakazi wa Kanda ya Kaskazini, kwenye uchaguzi huu tuunganishe nguvu zetu kwa sisi wenyewe kujitolea na muda wetu na rasilimali zetu, ili tuwashughulikie CCM ambao wamekuwa wakiendelea kuwatesa Watanzania kwa sera zao mbovu na uongozi wa kihuni ambao haujali kabisa maisha ya Watanzania.
Imetolewa na Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini
+255 754 912 914 au 0784 343 275


golugwa@gmail.com

Habari kwa hisani ya: Global Publisherstz

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 mchambuzi@habari online. Blogger Template by Bloggertheme9
Proudly Powered by Blogger.
back to top