Feb 1, 2014

Njaa yaitesa Sudan ya kusini;millioni 3.7 hawana chakula

Posted at  2/01/2014  |  in  Habari

Picha ya wahanga wa njaa sudan ya kusini

Umoja wa mataifa unakadiria kwamba takriban watu millioni 3.7 nchini Sudan kusini wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.
Akiongea na BBC Mratibu wa maswala ya kibinaadamu katika umoja huo Toby Lanzer alisema kwamba mzozo huo ulioanza mwezi Disemba mwaka jana umeharibu masoko pamoja na maisha ya kawaida ya watu, mbali na kusababisha hali mbaya ya kibinaadamu kwa thuluthi moja ya idadi ya raia.
Na ili kuzuia Janga ,amesema kuwa umoja wa mataifa unahitaji dola millioni 1.3 pamoja na mazingira yalio salama ili kutekeleza wajibu wake.
Maelfu ya raia wamepoteza maisha yao katika vita hivyo ambavyo umoja wa mataifa unasema vinaendelea licha ya kutiwa saini kwa mkataba wa kuvisitisha juma moja lililopita.

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 mchambuzi@habari online. Blogger Template by Bloggertheme9
Proudly Powered by Blogger.
back to top