Mbio za Liverpool zimeingia doa baada ya Kolo Toure kutoa pasi kwa adui aliyepachika goli la kusawazisha.
Wakiwa katika uwanja wa West Brom, Liverpool walianza vyema kwa kupachika bao lilifungwa na Daniel Sturidge kwa pasi safi ya Luis Suarez.
Walionekana kuutawala mchezo mapema kipindi cha kwanza na kuonekana kushinda kabla ya ndoto hizo kuota mbawa kipindi cha pili.
Mlinzi wa Liverpool Kolo Toure alitoa pasi mbovu ikaishia kwenye miguu ya anechebe aliyesawazisha goli. West Brom 1 - 1 Livepool.
Kwa mtaji huu safari ya kufuzu UEFA ni ngumu sana
ReplyDelete