Ni habari ya kusikitisha kwa Tanzania na raia wake "deni la taifa kufikia trilion 27".
Nchi iko katika wakati mgumu sana kwa kuwa na deni linalovuka asilimia hamsini ya mapato kwa mwaka.
Akiwa katika mahojiano kwa njia ya simu na Mohamed wa Redio BBC Swahili, mtaalamu wa uchumi duniani na mwenyekiti wa CUF nchini Profesa Ibrahim Lipumba alisikika akiwa na masikitiko makubwa sana.
Serikari ya awamu ya tatu iliacha deni likiwa trilion 5 na limeongezeka yaid ya mara nne katika kipindi kinachokaribia miaka 10.
Lipumba aliweka wazi wamba deni linazidi kuwa kubwa sababu kwa sababu mikataba mingi inazungukwa na misingi ya rushwa, kuibuka kwa miradi hewa na kutokuwa na misingi ya uwazi ndani yake.
Mwisho wa siku anayekuwa mhanga ni mwananchi wa kawaida kwani badala ya kutoa huduma za kijamii, pesa hushughulikia ulipaji wa deni.
yaan natamani kuitafuna serikali. ni aibu na tutakosa wawekezaji pia misaada
ReplyDeleteWameshatufanya sisi wajinga kwasababu hali ngumu hawagusi wao na familia zao,ni sisi makabwela tu
Delete