Ikiwa Emirates,Arsenal imefanikiwa kuipiga Crystal Palce 2 - 0.
Kukiwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha Arsene Wenger, Arsenal ilitawala mchezo dhidi ya Palace wanaocheza kwa ushirikiano mkubwa sana.
Bao la kwanza lilipachikwa nyavuni na kiungo Mwingereza Ox Chamberline alikuwa akicheza katikati leo kwa mpira mzuri uliomshinda kipa kimo.
Na alipachika goli la pili pia kwa pasi nzuri ya Santi Carzola.
Ushindi huo unaiweka Arsenal kileleni kwa muda huku ikingojea matokeo ya mchezo utakaochezwa kesho juma tatu kati ya Chelsea na Manchester City.
0 comments: