Kasisi mmoja huko Jamhuri ya Afrika ya kati anasema kuwa katika kipindi cha wiki moja takriban wakristo 75 wameuawa kutokana na ghasia baina ya vikundi vya kidini mjini Boda.
Alielezea kwamba Waisilamu waliojihami kwa silaha kali waliweka vizuizi katika mipaka ya kuingia na kutoka mjini humo kabla ya kuwashambulia wakristo.
Kasisi huyo ambaye amewapa hifadhi watu zaidi ya 1000 katika parokia yake alisema kwamba hajui ni waisilamu wangapi waliouawa kwa sababu miili yao ilizikwa muda mfupi baada ya kufa.
Maelfu ya watu wameuawa tangu vita hivyo kuzuka baada ya mapinduzi ya kijeshi ya serikali mwaka uliopita.
Kasisi Cassein Kamatari ametoa wito kwa majeshi ya kifaransa na yale ya Jumuia ya Africa kutoa usaidizi akisema kwamba watu wapatao 1500 wamepata hifadhi kanisani mjini Boda.
Mapigano hayo yalianza wiki iliyopita wakati ambapo wanamgambo wa kiislamu walipoanza kutoroka kuelekea Kaskazini. Watu waliojiami na walioripotiwa kuwa Waisilamu waliwaangamiza anagalau wakristo 75, hii ni kwa mujibu wa Kasisi Kamatari.
Ijapokuwa inakisiwa kwamba huenda Wakristo walihusika kwenye ghasia iazo, mengi kuhusu mapigano hayo bado hayajulikani.
Hayo yakijiri,mkuu wa mkuu wa kitaifa wa shirika la Msalaba Mwekundu amesema kuwa hangeweza kuhakiki takwimu za waliofariki lakini alisema kwamba kuna kikosi kilichotumwa mjini Boda kutafuta miili ya watu.
Alisema watu takriban 15 huuawa kila siku nchini humo.Hata hivyo kukizingatiwa idadi ya miji ambayo bado haijachunguzwa, idadi ya waliofaririki huenda ikawa ni zaidi.
0 comments: