Yatsenyuk anamtaka rais Putin kuamuru wanajeshi wake kurejea katika kambi zao na kuheshimu maafikiano ya Kimataifa kuhusu eneo hilo la Crimea.
Moscow inasema kuwa jeshi lake linawalinda raia wake katika mji huo ambao tayari majengo kadhaa ya serikali yamesimikwa na Bendera ya Urusi.
Viongozi wa Mataifa ya Magharibi wakiongozwa na rais wa Marekani Barrack Obama wameishtumu Urusi kuvamia Ukraine kijeshi na kutishia kusita uhusiano wao na Moscow ikiwa haitawaiondoa wanajeshi wake.
Hayo yanajiri wakati Urusi ikiendelea kutishia kuingilia kijeshi nchini Ukraine ambapo inaweza kuzuia mzozo mkubwa wa kimataifa ambao itakuwa ni hatari sana kuwahi kutokea tangu kuvunjika kwa muungano wa mataifa ya kikoministi.
Mataifa ya magharibi yanaendeleza shinikizo dhidi ya hatuwa ya Urusi kupeleka vikosi katika ardhi ya Ukraine ambayo itakuwa ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Mataifa hayo yanatishia pia kuiwekea vikwazo Urusi ambavyo miongoni ni kuitenga zaidi.
Vladimir Poutine bado anaendelea kuzua hali ya sintofahamu kufuatia nia yake, lakini katika mawasiliano kwa njia ya sim na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Poutine alikubali kuundwa kwa tume maalum itayo anzisha mazungumzo ya kisiasa nchini Ukraine.