Serikali ya Uganda imesema Bajeti yake ya mwaka huu wa 2014 haitaathirika ikiwa Mataifa ya Magharibi yatasitisha misaada ya kifedha kutokana na hatua ya rais Yoweri Museveni kusaini mswada unaopiga marufuku mapenzi ya jinsia moja nchini humo. Kampala inasema haitakuwa mara ya kwanza kwa Mataifa hayo kusitisha misaada.
0 comments: